PRISTINA: Ghasia za Kosovo zimesababisha vifo viwili | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PRISTINA: Ghasia za Kosovo zimesababisha vifo viwili

Watu 2 miongoni mwa wale 50 waliojeruhiwa katika mapambano ya siku ya Jumamosi katika mji mkuu wa Kosovo,Pristina,wamefariki kutokana na majeraha yao.Polisi wa kuzuia ghasia walifyatua gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya kama waandamanaji 3,000 waliokusanyika kupinga mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu mustakabali wa jimbo hilo ambalo ni sehemu ya Serbia.Wapinzani hao wanahisi kuwa mpango uliopendekezwa hivi karibuni na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa,Martti Ahtisaari haukuzingatia vya kutosha,kuipatia Kosovo uhuru wake.Kwa upande mwingine,Serbia inasema mpango huo umekwenda mbali mno.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com