PRISTINA : Bunge la Kosovo laridhia mpango wa uhuru | Habari za Ulimwengu | DW | 06.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PRISTINA : Bunge la Kosovo laridhia mpango wa uhuru

Bunge la Kosovo limeidhinisha kwa kauli moja mpango wa Umoja wa Mataifa ambao utalipatia jimbo hilo lenye wakaazi wengi wa asili ya Albania uhuru kutoka Serbia utakaokuwa chini ya usimamizi wa kimataifa.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 100 dhidi ya moja katika bunge lenye viti 120.Pendekezo hilo ambalo limeandaliwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa Martti Ahtisaari hivi sasa linajadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Serbia imeukataa mpango huo kwa kusema kwamba katu haitoiachilia Kosovo kwa hiari.

Urusi ambayo ni mshirika wa Serbia imedokeza kwamba huenda ikatumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama kuzuwiya mpango huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com