1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA:Mkutano wa EU na Afrika kuendelea hata waziri mkuu wa Uingereza asipohudhuria

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gr

Mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini na Ureno wamesema mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi na serikali wa Umoja wa Ulaya na Afrika unaopangiwa kufanyika mjini Lisbon nchini Ureno mwezi Desemba utandelea hata ikiwa waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown atakosa kuhudhuria.

Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini bibi Nkosazana Dlamini-Zuma amesema mkutano huo hautaathirika kwa kukosa kufika mtu mmoja.

Alikumbusha kuwa mkutano kama huo wa mwaka 2000 haukuhudhuriwa na waziri mkuu wa Uingereza wa wakati huo Tony Blair na pia waziri mkuu wa sasa Gordon Brown hakuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa wa mwezi uliopita.

Waziri wa mambo ya nje wa Ureno Luis Amado amesema itakuwa kosa kubwa kwa Umoja wa Ulaya kudhoofisha uhusiano wake na bara la Afrika.

Kamishna wa Umoja wa Ulaya Jose Barroso amesema msimamo wa bwana Brown hauzingatii haki na wala hakuna sababu ya kuutatiza mkutano huo kwa ajili ya mvutano wa Uingereza na Zimbabwe.