1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prague: Serekali mpya ya mseto inaundwa aktika Jmahuri ya Cheki.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHb

Katika Jamhuri ya Cheki, Rais Vaclav Klaus ameikubali serekali mpya ya mseto ya vyama vya mrengo wa kati na kulia, ikiongozwa na waziri mkuu, MirekTopolanek, baada ya kuweko mzozo uliodumi miezi saba. Mzozo huo ulitokana na uchaguzi ambao matokeo yake hayajawa wazi kabisa. Serekali ya vyama vitatu ya Bwana Topolanek ina siku 30 kupata kura ya kuwa na imani nayo bungeni. Serekali hiyo ina wabunge 100 kati ya 200, hivyo kubakia inawategemea waasi wa kutoka vyama vya mrengo wa shoto. Mwezi SEptemba mwaka jana. Bwana Topolanek alishindwa katika jaribio lake la kwanza la kuunda serekali.