PRAGUE: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ashauriana na Waziri Mkuu wa Czech | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PRAGUE: Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ashauriana na Waziri Mkuu wa Czech

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, ameshauriana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech, Mirek Topolanek, kuhusu katiba ya Ulaya, mjini Prague.

Bibi Merkel, baadaye alisema mazungumzo yao yalifana na kwamba Mirek Topolanek alitoa maoni kadhaa ya kuzingatiwa kuhusu jinsi ya kufufua katiba hiyo iliyokwama.

Bibi Angela Merkel, ambaye serikali yake inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya, amepania kushauriana na mataifa yote ishirini na saba wanachama wa Umoja huo kuhusu katiba hiyo iliyokataliwa na wapiga kura nchini Uholanzi na Ufaransa mwaka 2005.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com