1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Prabowo Subianto aapishwa kuwa rais wa Indonesia

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Indonesia imemuapisha Jenerali wa zamani wa jeshi Prabowo Subianto kuwa Rais mpya wa taifa hilo. Wakati wa hafla ya kuapishwa kwake Jumapili Rais Subianto amesisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa na ujumuishwaji.

https://p.dw.com/p/4lzxi
Prabowo Subianto aapishwa kuiongoza Indonesia
Rais mteule wa Indonesia (Kushoto) Prabowo Subianto na mtangulizi wake Joko Widodo katika hafla ya kumuapisha mjini JakartaPicha: Bay Ismoyo/AFP

Kiongozi huyo mpya wa Indonesia ameahidi pia kuwakilisha maslahi ya raia wote wa taifa hilo, bila kujali itikadi zao za kisiasa.Kiongozi huyo mpya aliyeahidi pia kuimarisha uchumi ameapishwa sambamba na makamu wake Gibran Rakabuming Raka mwenye miaka 37 ambaye ni mtoto wa kwanza wa rais aliyemaliza muda wake Joko Widodo.

Soma zaidi: Rais wa Indonesia ampongeza mshindi wa uchaguzi Prabowo

Mojawapo ya mambo anayotarajiwa kuyatekeleza rais Subianto na serikali yake atakayoiunda ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuanzisha programu ya chakula cha mchana bure mashuleni kuanzia Januari 2025. Mradi huo unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani milioni 53 kwa siku.