1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prabhakaran Kiongozi wa watamil auwawa .

19 Mei 2009

Ndoto ya kuwa na dola huru ya watamili imetoweka ?

https://p.dw.com/p/HtZB
Mahinda Rajapaksa-rais wa sri Lanka.Picha: AP

Baada ya kupita robo karne, yaonesha vita vya kienyeji kisiwani Sri Lanka vimemalizika.Kwa muujinu wa Jeshi la serikali, kiongozi wa waasi wa kitamili,VELUPILLAI PRABHAKARAN,ameuwawa wakati akijaribu kutoroka pamoja na viongozi wa jeshi lake . Jeshi la ukombozi la "Tamil-Tiger ", lilikwisha salim amri na kuridhia tangu jumapili kuwa ,ndoto yake ya kuunda dola huru la watamili haikutimilia.Kuuwawa kwa Kiongozi wa waasi wa Tamil-Tiger,kumeitikiwa vipi ?

Waziri mkuu wa Sri Lanka amethibitisha kuuwawa kwa Kiongozi wa waasi wa kitamili.

Hata watu mitaani ,wameshangiria kuuwawa kwa kiongozi wa waasi Prabhakaran.Tangu mwishoni mwa wiki pale rais wa Sri Lanka Mahinda Rajapakse ,aliponadi ushindi katika vita dhidi ya waasi wa Tamil Tiger, watu wakisherehekea katika mji mkuu Colombo na wakiwapa wanajeshi wao wali uliotiwa sukari.Msichana mmoja akasema:

"Nimefurahi kupita kiasi.Tumesubiri kitambo kirefu.Ninaishi tangu kuzaliwa kwangu na vita hivi.Na sikutaka kufa navyo."

Mtamili,dereva wa Taxi alisema kwamba, ulimwengu mzima daima ukisema kuwa ugaidi hauwezi kushindwa.Na sisi sote tukidhani hivyo.Tunatoa shukurani zetu kwa rais wetu na kwa jeshi letu.Sasa tunaweza pamoja na kizazi kijacho kuishi kwa amani-alisema mtamili huyo.

Masaa tu tangu kumalizika kumwaya damu msituni ,msemaji wa jeshi la serikali alitangaza juzi jumapili kuwa wapiganaji wa Tamil Tiger ama wasalim amri au wajiue binafsi.

Kwa muujibu wa taarifa zake, jeshi la serikali ya Sri Lanka lilimzingira kiongozi huyo wa waasi msituni huko kaskazini-mashariki mwa sri Lanka akiwa pamopja na wapiganaji wake kiasi cha 200.Aliuwawa wakati wa mapigano ya risasi na vikosi vya serikali .Kwa muujibu wa taarifa za jeshi la serikali,uongozi mzima wa jeshi lake umeuwawa.Miongoni mwao mtoto wake.Mtandao ulio karibu na waasi-TamilNet umedai kilichopita ni mauaji ya halaiki yaliofanywa n a majeshi ya serikali.

Kiongozi wa waasi Veluppillai Prabhakaran aliekuwa na umri wa miaka 55,akijitokeza nadra tu hadharani.Aliunda jeshi la waasi la chui wa kitamil kutoka Tamil Eelam (LITTE) kwa ufupi ,kutokana na chama cha vijana cha chama hicho hapo 1976.Mwanzoni mwa miaka ya 1980,Tamil Tiger wakaanz kushika silaha ili kuunda nchi ya watamili-jamii ya wachache kisiwani sri Lanka waliohisi wakikandamizwa kaskazini na mashariki ya kisiwa hicho.

Mtayarishaji: Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdul-Rahman