1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

POTSDAM:Mawaziri wa G8 waonya juu ya mikopo yenye madhara kwa Afrika

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC09

Mawaziri wa fedha wa mataifa nane tajiri duniani wameonya dhidi ya mikopo isiyo na manufaa inayotolewa kwa nchi za afrika, ambayo inakuwa migumu kulipika.

Lakini hata hivyo mawaziri hao wamesema kuwa ni lazima nchi hizo za kiafrika zibebe jukumu la kudhibiti matumizi ya fedha hizo.

Mawaziri hao wa fedha wa kundi la mataifa nane, walitoa taarifa hiyo mwishoni mwa mkutano wao wa siku mbili hapo jana huko katika mji wa Potsdam hapa Ujerumani.

Wamesema kuwa Afrika itakuwa ajenda muhimu katika mkutano ujayo wa wakuu wa kundi hilo la G8 huko Heiligendamm katika pwani ya Baltic.

Ujerumani iliitolea mfano China ambayo imesema kuwa imekuwa ikifyonza utajiri wa mafuta barani afrika kwa ajili ya uchumi wake unaokua kwa kasi.