1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Potsdam , Ujerumani. Marekani na Russia zatupiana maneno.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwN

Marekani na Russia zimevutana kuhusiana na mpango wa Marekani wa kuweka ngao dhidi ya makombora mpango unaotarajiwa kujengwa katika bara la Ulaya.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice , ambao wanahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la mataifa tajiri yenye viwanda duniani G8 katika mji wa Potsdam nchini Ujerumani , walishambuliana kwa maneno kuhusiana na mpango huo wa Marekani utakaowekwa katika eneo la Ulaya ya mashariki.

Hapo mapema , Rice alieleza wasi wasi wa Russia kuhusiana na ngao hiyo kuwa wa kipuuzi.

Kumekuwa pia na kutokukubaliana juu ya hali ya baadaye ya jimbo la kosovo. Marekani inakubaliana na kulipatia jimbo hilo uhuru kutoka Serbia, suala litakaloangaliwa na jumuiya ya kimataifa, mpango ambao unapingwa mno na Russia.

Mkutano huo wa Potsdam ulikuwa na lengo la kuchambua ajenda za mkutano wa viongozi wa kundi la G8 unaotarajiwa kufanyika nchini Ujerumani mwezi ujao.