1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

POTSDAM: Nchi za Kiafrika zikingwe dhidi ya madeni mapya

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0d

Waziri wa fedha wa Ujerumani,Peer Steinbrück ametoa wito wa kuwepo uwazi zaidi duniani katika sekta ya akiba ya kinga.Steinbrück,alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri wa fedha wa nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda G-8. Akasisitiza juu ya haja ya kuwa na mfumo wa maadili,kuhusu fuko la akiba ya aina hiyo.Mkutano huo,nje ya mji wa Potsdam,mashariki mwa Ujerumani unatayarisha mkutano wa kilele wa G-8 utakaofanywa mwezi ujao katika mji wa pwani wa Heiligendamm,kaskazini mwa Ujerumani.Baadae hii leo,mawaziri wa fedha wanatazamiwa kukubaliana na mpango ulio na azma ya kuzikinga nchi za Kiafrika dhidi ya mzigo wa madeni mapya.