1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Misri yaanza kuwazuia wapalestina kuvuka kiholela mpaka wake wa Rafah

26 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cy0M

RAFAH:

Polisi wa kuzuia fujo wa Misri wameanza kuzuia magari yanayotoka Gaza na kuingia Misri.Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya wapiganaji wa kundi la Hamas kutoboa tundu lingine katika ukuta unaotenganisha Gaza na Misri hiyo jana.Mamia ya polisi wa kuzuia fujo wamejipanga msururu mmoja kuzuia njia ambazo zilikuwa zinatumiwa na magari.Askari hao wanasaidiwa na vifaru vya jeshi la Misri kuweka doria.Lakini mapema leo vikosi vya usalama vya Misri viilikuwa vimerejea nyuma kutoka mpaka wa nchi hiyo na Gaza baada ya kushindwa kuuziba tena.Wapalestina wakati huo walionekana kama baado wanaendelea kuvuka mpaka bila kuzuiliwa,kuingia na kutoka Misri kwa siku ya mfululizo.Wapalestina wanafanya hivyo ili kujilimbikizia bidhaa muhimu kwa maisha yao baada ya kuwekewa mzingiro na Israel ambao hivi karibuni ulitishia kusababisha janga la kibinadamu.Tingatinga hapo awali lilitoboa tundu lingine katika ukuta wa mpaka,baada ya vikosi vya Misri kufaulu kuziba matundu mengine yaliyotobolewa hapo awali.

Kwa mda huohuo,baado kuna utata katika taarifa kuwa rais wa Misri amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano wa makundi ya kipalestina yanayohasiamiana.Kundi la Hamas ,ambalo linadhibiti Gaza,linaonekana kukubali mwito huo,lakini wizara ya mashauri ya kigeni ya Misri imeziita taarifa hizo kama sio na ukweli.Hata hivyo mipango imetangazwa ya mkutano kati ya waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas kujadilia mgogoro huo.