1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Kenya yasema idadi ya waliokufa katika ghasia imefika 700

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Coxv

NAIROBI:

Idadi ya watu ambao wamepoteza maisha yao katika ghasia za kisiasa na kikabila nchini Kenya sasa imepita 700.

Afisa wa juu wa jeshi la polisi ameliambia shrika la habari la AFP kuwa idadi ya wahanga nchini kote ni zaidi ya 700.

Hii imefuatia taarifa za kugundulika miili mingine 85 katika mikoa ya Rift Valley na magharibi.

Kupanda kwa idadi ya waliopoteza maisha yao imekuja wakati katibu mkuu wa Umoja wa Matiafa-Ban Ki-moon kuwaonya rais Mwai Kibaki pamoja na kiongozi wa upinzani-Raila Odinga,kuwa wakishindwa kupata ufumbuzi wa mgogoro huo kutakuwa na madhara makubwa.

Odinga anakataa kukubali kuwa Bw Kibaki alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi jana akidai kuweko kwa mizengwe.

Aidha amekataa kuka katika meza moja na hadi pale Bw Kibaki atakapo kiri kuwa kulikuwa na wizi katika uchaguzi.Amesisitiza kuwa maandamano yataendelea nchini humo.

Kibaki jumamosi amesisitiza umuhimu wa viongozi wa kisiasa kuwahudumia wakenya wote.

Watu karibu laki mbili Unusu waliachwa bila makazi wengi wakiwa katika mkoa wa Rift valley. Chama cha msalaba mwekundu cha Kenya kilionya jumamosi kuwa hali ya watu hao ni mbaya sana.