1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Ujerumani yavunjwa soko haramu la mtandaoni

Iddi Ssessanga
12 Januari 2021

Jeshi la polisi nchini Ujerumani imevunja mtandao wa tovuti za siri maarufu kama Darknet, ambako biashara haramu ya uuzaji wa madawa ya kulevya, data zilizoibwa na programu za udukuzi wa computer imekuwa ikifanyika.

https://p.dw.com/p/3npYe
Deutschland Prozess um Darknet Cyberbunker gestartet
Picha: Harald Tittel/dpa/picture-alliance

Katika wakati wa kufungwa kwake, soko hilo la siri la mtandaoni lilikuwa na watumiaji karibu 500,000 na zaidi ya wauzaji 2,400 kutoka kote duniani, wakati ambapo janga la virusi vya corona limepelekea sehemu kubwa ya biashara ya madawa mitaani kuhamia mtandaoni.

Waedesha mashtaka wamesema polisi katika mji wa kaskazini wa Oldenburg walifanyikiwa kumkamata mtu anaedaiwa kuwa mwendeshaji wa mtandao huo mwishoni mwa wiki.

Taarifa imeongeza kuwa wachunguzi waliweza pia kulifunga soko na kuzima server yake siku ya Jumatatu, wakiitaja hatua hiyo kuwa hitimisho la operesheni ya kimataifa iliyodumu kw amiezi kadhaa.

Darknet Shop
Mwanaume akiwa kwenye tovuti ya duka la mtandaoni linalouza silaha za rasharasha kwenye soko la Darknet mjini Rottweil, Ujerumani.Picha: Silas Stein/dpa/picture alliance

Jumlya ya miamala isiopungua 320,000 ilifanyika kupitia soko hilo haramu la mtandoani, ikiwemo miamala zaidi ya 4,650 ya sarafu za mtandaoni maarufu bitcoin na 12,800 ya monero - ambazo ni sarafu mbili miongoni mwa sarafu maarufu zaidi za mtandaoni zinazouzwa sana.

soma pia: Kompyuta na Mtandao wa Internet –Kipindi 2 – Kununua kompyuta

Kwa viwango vya sasa vya ubadilishaji fedha, miamala hiyo iliwakilisha biashara yenye thamani ya euro milioni 140, sawa na dola la Marekani milioni 170.

Biashara zinazofanyika darknet

Mtandao huo ulitoa huduma za mauzo ya kila aina ya madawa ya kulevya, pamoja na pesa bandia, data bandia na zilizoibwa za kadi za fedha, simukadi za siri, programu za udukuzi na mambo mengine mengi tu.

Raia wa Australia mwenye umri wa miaka 34 anaeaminika kuwa mwendeshaji wa mtandao huo wa DarkMarket, alikamatwa karibu na mpaka wa Ujerumani na Denmark, mara baada ya kukamatwa kwa server zaidi ya 20 zilizokuwa zinatumika nchini Moldova na Ukraine.

Screenshot Angebot im Darknet
Baadhi ya bidhaa zinazoizwa kwenye duka la siri la mtandaoni, yakiwemo madawa ya kulevya, sarafu za mtandaoni na mambo mengine.

Wachunguzi wanatazamia kutumia data zilizohifadhiwa katika server hizo kuanzisha uchunguzi mpya dhidi ya waongozaji, wauzaji na wanunuzi kwenye soko hilo la siri la mtandaoni. Mshukiwa mkuu alifikishwa mbele ya jaji lakini alikataa kuzungumza.

Soma pia: Sheria ya makosa ya mtandao yaanza Tanzania

Kitendo cha usimamizi wa sheria ya madawa katika idara ya upelelezi wa ndani nchini Marekani, FBI, na mamlaka ya kodi IRS, zilishiriki katika uchunguzi huo pamoja na polisi kutoka Australia, Uingereza, Denmark, Uswisi, Ukraine na Moldova, huku shirika la polisi barani Ulaya Europol, likitekeleza jukumu la uratibu wa operesheni nzima.

Mtandao wa siri wa darknet, unahusisha tovuti ambazo zinaweza kuingiwa tu kwa kutumia programu au idhini makhsusi, na hivyo kuhakikisha usiri wa watumiaji.

Chanzo: AFPE