Polisi Ujerumani wapinga kuondosha udhidbiti mpakani | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi Ujerumani wapinga kuondosha udhidbiti mpakani

Mamia ya maafisa wa polisi Ujerumani ya mashariki wamepinga mipango ya kuondowa udhibiti wa mipakani mwezi ujao.

Chama cha wafanyakazi cha polisi kinamtaka Waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble kuendelea kuwabakisha polisi wa serikali ya shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwenye mpaka hadi hapo utakapokuwa umefanyika uchambuzi wa usalama unaoaminika.

Schäuble amezikataa shutuma hizo kwa kusema kwamba kufunguliwa mpaka kwa nchi jirani za mashariki hakutopunguza kiwango cha usa lama nchini Ujerumani.

Schäuble anasema hiyo ni dhamira njema kwamba tarehe hiyo 21 Desemba italeta uhuru wa kiwango kikubwa lakini sio uchache wa usalama kwa watu wa pande mbili za mpaka na utakuwepo usa lama zaidi na maalum.

Upingaji huo usio ya kawaida wa polisi unaonyesha hof u nchini Ujerumani juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa uhalifu au kumiminika kwa wimbi kubwa la wahamiaji wasio halali wakati mpaka huo utakapofunguliwa hapo tarehe 21 Desemba.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com