1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi la Tanzania latuhumiwa kutumia nguvu

10 Januari 2011

Chama cha wanasheria wa Tanzania kinalaani kisa hicho kilichoppelekea viongozi kadhaa wa chama cha upinzani CHADEMA walikamatwa.

https://p.dw.com/p/zvmJ
Rais wa Tanzania Jakaya KikwetePicha: DW

Chama wanasheria nchini Tanzania-TLS, kimesema kuwa polisi walitumia nguvu nyingi dhidi ya raia wakati walipozuia maandamano wiki iliyopita. Mwenyekiti wa chama hicho, Felix Kibodya, leo amelaani vikali hatua hiyo iliyochukuliwa na jeshi la polisi, katika kuwanyima haki ya kikatiba ya mikutano na kujieleza.

Kibodya amesema kuwa chama chake kinalaani vikali matumizi hayo ya nguvu ya kuwatawanya waandamanaji wasio kuwa na silaha ambao walikuwa wakiandamana kwa amani. Siku ya Jumatano watu watatu waliuawa mjini Arusha, baada ya polisi kuwafyetulia risasi waandamanaji wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, waliokuwa wanaipinga serikali.

Viongozi kadhaa na wafuasi wa CHADEMA, walikamatwa katika maandamano hayo. Hata hivyo, siku ya Ijumaa, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania aliwaambia mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa yaliyoko mjini Dar es Salaam, kuwa amesikitishwa sana na mauaji hayo.