Polisi 5 wauwawa Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 09.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi 5 wauwawa Irak

BAGHDAD

Taarifa kutoka Baghdad,nchini Irak zinasema kwamba wapiganaji kadhaa waliokuwa na bunduki walihujumu kituo cha polisi katika kijiji kinachokaliwa mno na waumini wa madhehebu ya Sunni huko kaskazini mwa Irak hii leo na kuua askari 5 kabla hawakutimuliwa kwa msaada wa wakaazi wa huko.Washambulizi waliendesha mgari 10 kutoka magharibi mwa Irak hadi kwenye kijiji hicho cha Hajaj na kufyatua risasi katika kituo hicho cha polisi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com