Poland kutia saini mkataba wa Lisbon | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.10.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Poland kutia saini mkataba wa Lisbon

Rais wa Poland Lech Kaczynski anatarajiwa leo hii kutia saini mkataba wa umoja wa Ulaya unaojulikana kama mkataba wa Lisbon.

default

Rais wa Poland Lech Kaczynski ambaye hatimaye ataidhinisha mkataba wa Lisbon leo.

Rais wa Poland Lech Kaczynski hii leo atatia saini mkataba wa Umoja wa Ulaya uliyofanyiwa marekebisho na kujulikana kama Mkataba wa Lisbon. Sherehe hiyo katika ofisi yake mjini Warsaw inatazamiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Bunge la Ulaya Jerzy Buzek, Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso na Waziri Mkuu wa Sweden Fredrik Reinfeldt.

Mkataba wa Lisbon ulikwisha idhinishwa na mabunge yote mawili ya Poland tangu mwezi wa Aprili. Lakini Kaczynski aliamua kungojea matokeo ya duru ya pili ya kura ya maoni nchini Ireland kabla ya kutia saini mkataba huo. Poland na Jamhuri ya Czeki ni nchi mbili za mwisho katika Umoja wa Ulaya zinazosubiriwa kutia saini mkataba huo.

Sasa Rais wa Jamhuri ya Czeki Vaclav Klaus anapaswa kutia saini yake ili Mkataba huo wa Lisbon uweze kutumika.

 • Tarehe 10.10.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/K3T0
 • Tarehe 10.10.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/K3T0
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com