1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Platini akosa kufika mbele ya kamati ya FIFA

18 Desemba 2015

Michel Platini, hakufika mbele ya kamati ya maadili ya FIFA wakati wa kikao cha kusikiza kesi ya malipo ya dola milioni mbili ambayo rais huyo wa UEFA alipokea 2011 kwa kazi ya FIFA iliyofanywa mwongo mmoja kabla

https://p.dw.com/p/1HQAW
Michel Platini
Picha: Getty Images/P. Schmidli

Uamuzi wa kesi hiyo unaotarajiwa Jumatatu, utaamua ikiwa Platini anaweza kugombea wadhifa wa rais wa FIFA katika uchaguzi wa Februari 28.

Platini alisema kupitia mawakili wake kuwa hangehudhuria kwa sababu alihisi tayari kesi hiyo ilikuwa ishaamuliwa kutokana na matamshi ya karibuni yaliyotolewa na msemaji wa jopo la uchunguzi Andreas Bantel. Aidha alisema kesi hiyo inayomkabili ni ya kisiasa kwa sababu inalenga kumzuia kuwania urais wa FIFA.

Platini anawakilishwa na timu yake ya mawakili katika kesi hiyo, siku moja baada ya rais wa FIFA Sepp Blatter kufika mbele ya kamati hiyo kuhusiana na “malipo yasiyo ya uaminifu” ya mwaka wa 2011 ambayo yanachunguzwa na waendesha mashtaka wa Uswisi. Malipo hayo yalisababisha Blatter na Platini kusimamishwa kazi na FIFA kwa siku 90 mwezi Oktoba.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu