Pistorius abubujikwa machozi mahakamani | Michezo | DW | 15.02.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Pistorius abubujikwa machozi mahakamani

Mwanariadha wa Afrika Kusini ambaye ni bingwa wa Olimpiki kwa walemavu Oscar Pistorius ametiririkwa machozi mahakamani wakati wakati akikanusha kuwa alimuuwa mchumbake kwa kumpiga risasi.

epa03585062 South African paralympic and Olympic sprinter, Oscar Pistorius (C) weeps as he appears in the Pretoria magistrates court after spending the night in police custody in Pretoria, South Africa 15 February 2013. Pistorius has been officially charged with murder. He was arrested 14 February 2013 for allegedly shooting and killing his girlfriend Reeva Steenkamp at his home in the Silverwoods security estate in Pretoria, South Africa. EPA/Antoine de Ras SOUTH AFRICA OUT

Oscar Pistorius Freundin Südafrika Gericht Schüsse Tod

Waendesha mashitaka wamesema watamfungulia mashtaka ya mauwaji ya kutokusudiwa aliyofanya dhidi ya mchumbake, mwanamitindo Reeva Steenkamp ambaye alipigwa risasi na kuuawa nyumbani kwa Oscar karibu na mji wa Pretoria Alhamisi iliyopita.

Ombi la kutaka awachiliwe kwa dhamana liliahirishwa hadi Jumanne ijayo na hivyo basi Pritorius angali kizuizini. Wapelelezi wanaendelea kutafuta ushahidi nyumbani kwa mwanariadha huyo ambako mwathriiwa, Steenkamp mwenye umri wa miaka 29 alifariki. Pistorius aliandikisha historia jijini London mwaka uliopita wakati alipokuwa mwanariadha wa kwanza mwenye ulemavu wa miguu kushindana katika mashindano ya Olimpiki. Pistorius na Steenkamp wanaripotiwa kuchumbiana tangu mwezi Novemba mwaka jana.

Visa vingine kama hivyo

Oscar Pistorius akipelekwa katika kizuiz cha polisi baada ya kutokea mauwaji nyumbani kwake

Oscar Pistorius akipelekwa katika kizuiz cha polisi baada ya kutokea mauwaji nyumbani kwake

Hicho hakijakuwa kisha cha kwanza ampaon mwanamichezo amehusika na mauwaji ya aina hiyo au majaribio ya mauwaji ya rafiki, jamaa au mtu mwingine…

Na mnamo Desemba mwaka wa 2012, mchezaji wa soka ya Wamarekani yaani American Football wa klabu ya Kansas City Chiefs Jovan Belcher alimpiga risasi na kumuuwa mchumbake na kisha akajitoa uhai. Polisi ilisema walikuwa na mgogoro kabla.

Novemba mwaka wa 2004, mchezaji wa mchezo wa magongo ya barafu wa klabu ya St Louis Blues Mike Danton alihukumiwa kifungo cha miaka saba na nusu gerezani kwa kupanga njama ya mauwaji. Alipatikana kwa kujaribu kumlipa jambazi ili amuuwe wakala wake Mike Frost, kwa madai ya kumdhulumu kakake mdogo Dalton.

Juni mwaka wa 1994, mke wa zamani wa aliyekuwa mchezaji wa American Football OJ Simpson, Nicole Brown Simpson, na rafiki yake walipatikana wamekufa. Simpson akashtakiwa kwa mashitaka mawili ya mauwaji lakini akaachiliwa huru kutokana na utata wa hali ya juu ulioikumba kesi hiyo.

Lewandoswki kujitetea mbele ya kamati ya nidhamu

Robert Lewandowski anaendelea kuwa na msimu mzuri katika klabu yake ya Borussia Dortmund

Robert Lewandowski anaendelea kuwa na msimu mzuri katika klabu yake ya Borussia Dortmund

Katika habari za soka ya hapa Ujerumani Bundesliga, mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund Robert Lewandowski atafika mbele ya kamati ya kinidhamu ya shirikisho la soka Ujerumani DFB Jumanne wiki ijayo katika jaribo la kubatilisha adhabu yake ya kutocheza mechi tatu za Ligi.

Lewandowski alipigwa marufuku kutokana na kadi yake ya kwanza nyekundu aliyopata wakati wa kichapo walichopata cha magoli manne kwa moja dhdi ya Hamburg mwishoni mwa wiki iliyopita na leo hatacheza mechi yao dhidi ya Eintracht Frankfurt. Huku akiwa na magoli 14 katika mechi 20 za Bundesliga, mshambuliaji huyo raia wa Poland ndiye mfungaji bora wa Dortmund nsimu huu na mkufunzi wake Jurgen Klopp angependa kuwa naye katika mechi dhidi ya Borussia Moenchengladbach na Hanover 96 katika wiki chache zijazo.

Klabu ya Schalke 04 inataraji kuwa na mshambuliaji wake Mholanzi Klaas-Jan Huntelar kwa mchuano wa Jumatano wiki ijayo wa awamu ya timu 16 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray. Mshambuliaji huyo ametemwa katika kikosi kitanachocheza mchuano wa leo wa Bundesliga dhidi ya Mainz 05 baada ya kukosa pia mchuano ambao Schalke waliwazabwa magoli manne kwa sifuri na viongozi Bayern Munich Jumamosi iliyopita, kutokana na tatizo la jicho na sas ahuenda asicheze tena mjini Istanbul Jumatano ijayo. Schlake pia watakosa huduma za beki Mjapan Atsuto Uchida wakati wa mchuano wa leo dhidi ya Mainz baada ya mchezaji huyo kurejea kutoka kibaria cha taifa lake akiwa na jeraha la goti. Aidha mchezaji wa pembeni mholanzi Ibrahim Affeley na beki wa Ugiriki Kyriakos Papadopoulos wako mkekani wakiuguza majeraha.

Nao Bayern Munich wanasubiri kusikia habari nzuri za kiungo wao Mhispania Javier Martinez kabla ya kipute chao cha Jumanne dhidi ya Arsenal. Mchezaji raia wa Brazil, Luiz Gustavo anatarajiwa kujaza pengo pamoja na Mjerumani Bastian Schweinsteiger. Claudio Pizarro, mshambuliaji nambari tatu nyuma ya Mario Mandzukic na Mario Gomez pia wanajizatiti kuwa katika hali nzuri kiafya kabla ya pambano hilo kutokana na maumivu ya koo.

Mwandishi: Bruce Amani/reuters/AFP/DPA

Mhariri: Mohamed Abdulrahman