1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

​​​​​​​Pirlo aanza taaluma ya ukocha kwa ushindi

Bruce Amani
21 Septemba 2020

Juventus imeanza kuwinda taji lao la kumi mfululizo la ligi kuu ya Italia - Serie A kwa ushindi rahisi wa 3 - 0 dhidi ya Sampdoria wakati Andrea Pirlo akianza taaluma yake ya ukocha kwa ushindi

https://p.dw.com/p/3inmk
Fussball I Juventus v Sampdoria - Allianz Stadium
Picha: Jonathan Moscrop/empics/picture-alliance

Andrea Pirlo ameanza taaluma yake ya ukocha kwa ushindi baada ya Juventus kuanzisha kampeni ya kubeba taji la ligi la 10 mfululizo na ushindi wa 3 - 0 dhidi ya Sampdoria jana.

Pirlo amesema hataki kumuiga yeyote katika aina yake ya mchezo. Muitaliano huyo kiungo wa zamani wa Juve aliyepokea kibali chake cha ukocha wiki iliyopita, amewataja Pep Guardiola, Carlo Ancelotti na Antonio Conte. Amesema anataka kutumia mawazo yake binafsi na atachukua mfano kutoka kwa timu zilizomfurahisha.