Pigo kwa kamati ya maandalizi ya riadha London | Michezo | DW | 12.02.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Pigo kwa kamati ya maandalizi ya riadha London

Kamati ya maandalizi ya michezo ya London ya riadha duniani mwaka wa 2017, ilipigwa na pigo jingine wakati afisa mwengine alipojiuzulu, akiwa ni watatu katika kipindi kisichozidi wiki moja

Hii ni baada ya Mkurugenzi msimamizi Sally Bolton naye kufungasha virago. Katika taarifa yake Bolton aliyejiunga na kamati hiyo 2014 hakueleza sababu za kujiuzulu, zaidi tu ya kusema , “ Ninafuraha kubwa mno kwa kazi iliokamilishwa katika kupata mafanikio na mapema ya kuweka msingi kwa ajiliv ya mafanikio ya mashindano hayo.”

Mnamo Wiki iliopita wajumbe wawili wa kamati hiyo, makamu mwenyekiti Heather Hancock na mwenyekiti wa kamati ya mahesabu Martin stewart pia walijiuzulu, kukiwa na ripoti za kuwepo na tafauti kati ya bodi na Mwenyekiti wa maandalizi ya michezo hiyo ya London 2017, ed warner ambaye pia ni Mwenykiti wa Chama cha riadha cha Uingereza.

Mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia , mhimili wa Shirikisho la vyama vya riadha la Kimataifa –IAAF, yatafanyika London ikiwa mara ya kwanza kufanyika jijini humo ,kuanzia Agosti 5 hadi 13, 2017.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com