Pigo jingine kwa rais Musharraf | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Pigo jingine kwa rais Musharraf

Katika kile kinachoonekana kama pigo jipya kwa utawala wa rais Pervez Musharaff wa Pakistan,waziri anayehusika na technolojia ya habari nchini humo Ishaq Khan Khakwani amejiuzulu. Ishaq anasema hatua hiyo ni katika kupinga rais Musharaf kuendelea kubakia madarakani.

Rais Musharraf akiwa ziarani Kashmir

Rais Musharraf akiwa ziarani Kashmir

Musharraf ambaye aliingia madarakani kufutia mapinduzi ya kijeshi ya umwagikaji damu mwaka wa 1999, anataka kuchaguliwa tena kuwa rais .Kati ya mwezi ujao au mwezi september ananuia kuwaomba wabunge wampe awamu nyingine ya miaka mitano kabla ya muhula wake kama amiri jeshi mkuu kumalizika baadaye mwaka huu.

Uamuzi huo umeanza kuwakera wengi hasa walioko katika serikali yake.Waziri anayehusika na technolojia ya habari Ishaq Khan Kwakwani amesema japokuwa amejizulu kutoka serikali atabakia mwaminifu kwa chama tawala nchini humo Pakistan Muslim leaque-PML-Q.

Akizungumza na wanahabari wa AFP Khakwami amesema musharraf napasa kuchaguliwa tena kutokana na utendakazi wake bali si kuwashinikiza wabunge kufanya hivyo.Pia alikanusha madai na baadhi ya vyombo vya habari kuwa alishinikizwa kujizulu kama waziri na maafisa wakuu.

Katika pigo jingine kwa serikali ya Rais musharraf mbunge Syed Ali Hasan Gilani ambaye pia ni katibu wa bunge kuhusu sayansi na technolojia ametangaza kuwa atakihama chama tawala cha PML-Q na kujiunga na chama pinzani cha aliyekuwa waziri mkuu Nawaz Sharif.

Musharraf alikabiliwa na tatizo jingine wiki iliyopita baada ya mahakama kuu kupinga uamuzi wa rais musharraf kumtimua jaji mkuu nchini humo.

Wapinzani wa rais musharraf wanasema kuwa kuchaguliwa kwake tena akiwa mwanajeshi ni jambo lisiloruhusiwa na itakuwa kinyume na katiba ya taifa hilo.Musharraf aliipindua serikali ya Sharif mwaka wa 1999 baada ya waziri huyo mkuu wa zamani kujaribu kumfuta kazi kama kiongozi wa kijeshi.

Inadaiwa kuwa Musharraf mara kwa mara amekuwa akiwatuma washauri wake jijini London kukutana na Benazir Bhutto ambaye pia ni waziri mwingine mkuu wa zamani nchini Pakistan, katika kile kinachokisiwa kama kujaribu kufikia makubaliano ya kugawana mamlaka.

Bhutto hata hivyo amesema waziwazi kuwa hawezi kushirikiana na rais Musharraf hadi ajiondoe kwenye jeshi. Bhutto na Sharif wamesema wanataji kurejea nchini Pakistan kushirika katika uchaguzi mkuu wa urais unaotarajiwa mapema mwaka ujao.

 • Tarehe 28.08.2007
 • Mwandishi Jane Nyingi
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH8x
 • Tarehe 28.08.2007
 • Mwandishi Jane Nyingi
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CH8x

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com