1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Picha 5
Lilian Mtono
10 Septemba 2019
https://p.dw.com/p/3PKdo

Mhariri wa picha wa Mexico Guillermo Arias ameshinda tuzo ya kifahari ya Visa d'Or ya picha za habari kutokana na taswira aliyoitoa ya msafara wa wahamiaji wa Amerika ya Kati.

Arias wa shirika la habari la AFP alitunukiwa tuzo hiyo kufuatia hadithi yake inayoitwa "Msafara" katika tamasha kubwa la kila mwaka la picha bora, shindano ambalo huandaliwa na The New York Times, shirika la habari la Reuters na The Washington Post.

Katika nyakati tofauti za 2018 na 2019, misafara ya wahamiaji na maelfu ya watu walienda njia ya kaskazini kutoka Amerika ya Kati. Wengi walikuwa wakielekea mpaka wa Merikani wakijaribu kuukimbia umasikini na vurugu katika nchi zao.

Marekani ilijibu hatua hizo kwa kutuma vikosi vya usalama wa mpakani. Washington pia ilianzisha kambi za kuwashikilia wale wanaovuka mpaka kinyume cha sheria, na kuweka sera ya ambayo watoto walitengwa na familia zao.