Peshawar.Maafisa nchini Pakistan wailaumu serikali kwa shambulio la wanafunzi. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Peshawar.Maafisa nchini Pakistan wailaumu serikali kwa shambulio la wanafunzi.

Waandamanaji na maofisa nchini Pakistan wameilaumu Marekani kwa mashambulizi ya anga hii leo ambayo jeshi lilidai limewauwa kiasi cha watu 80 wanaoshukiwa kuwa ni wanamgambo waliokuwepo katika kambi ya kigaidi.

Siraj-ul-Haq, naibu waziri kiongozi wa jimbo linaloongozwa na waislamu la Kaskazini Magharibi amejiuzulu baada ya kufanywa shambulio hilo katika shule ya kidini karibu na mpaka na Afghanistan.

Akielezea sababu za kujiuzulu kwake Siraj-al-Haq amesema ni kutokana na kuonyeshahuzuni zake dhidi ya shambulio lililouwa wanafunzi 80 wasio na hatia yoyote.

Siraj aliyehudhuria mazishi ya wanafunzi 20 kati ya waliouliwa hii leo katika Jimbo la Bajaur ameongeza kuwa, wengi wa waliouwawa ni watoto wadogo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com