1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESHAWAR: Wanamgambo wafutilia mbali maafikiano ya amani

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiP

Nchini Pakistan,wanamgambo wanaowaunga mkono Wataliban katika eneo linalopakana na Afghanistan wamefutilia mbali makubaliano ya amani yenye utata,yaliotiwa saini pamoja na serikali mwaka uliopita.Hati iliyotolewa na viongozi wa baraza la kundi la Taliban Shoora imepinga harakati mpya za kijeshi.Hali ya mvutano imezidi kuwa mbaya,tangu Msikiti Mwekundu unaowaunga mkono Wataliban,kuvamiwa na majeshi ya serikali ya Pakistan mjini Islamabad,juma lililopita.Mapema hii leo shambulizi la pili la bomu dhidi ya msafara wa kijeshi,katika kipindi cha saa 24 limeua si chini ya wanajeshi na raia 14 kaskazini-magharibi ya Pakistan.Siku ya Jumamosi, wanajeshi 24 waliuawa katika shambulio la kujitolea muhanga dhidi ya msafara mwingine wa kijeshi.