1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESHAWAR: Maafisa wa Pakistan wachinjwa na Wataliban

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CO

Wanamgambo wanaowaunga mkono Wataliban,wamewakata vichwa maafisa wanne wa usalama wa Pakistan. Maafisa hao walitekwa nyara pamoja na watu wapatao kama darzeni moja,katika eneo la mvutano, kama kilomita 50 kutoka mji wa Peshawar, kaskazini ya Pakistan.

Kwa mujibu wa polisi,mauaji hayo yalitokea katika mapambano yaliyomlenga kiongozi mwenye itikadi kali za Kiislamu,Maualana Fazlullah,alietoa mwito kwa wafuasi wake kuanzisha vita vya jihad dhidi ya wanajeshi wa Pakistan.