Pengo kati ya maskani na tajiri duniani linaongezeka | Masuala ya Jamii | DW | 31.10.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Pengo kati ya maskani na tajiri duniani linaongezeka

Watu 116 millioni kutoka mataifa 131 duniani waomba umaskini utokomezwe

Sultani wa Sokoto,kulia na Waziri wa mashauri ya nje wa Ujerumani Walter Steinmeier, kushoto.Sultan aliomba haki sawa kwa wanawake

Sultani wa Sokoto,kulia na Waziri wa mashauri ya nje wa Ujerumani Walter Steinmeier, kushoto.Sultan aliomba haki sawa kwa wanawake

Takwimu rasmi zinaonyesha kama pengo kati ya watu maskini na matajiri duniani linazidi kuongezeka.Hali hiyo imepelekea wanaharakati kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua muafaka ili kuweza kuliziba.Wanaharakati wanadai kuwa serikali kadhaa zimeshindwa kuipaka kipa umbele mikakati ya kuutokomeza umaskini.

Watu zaidi ya millioni 116 kutoka nchi 131 duniani kote walishiriki katika kampeini ya kupambana dhidi ya umaskini duniani.Chini ya kauli mbiu 'jitokeze na chukua hatua' wachambuzi wanasema hiyo ndiyo kampeini kubwa kuwahi kuwahamasisha watu wengi kiasi hicho kuhusu suala moja.

Mashirika mawili, moja likijiita 'mwito wa kupambana dhidi ya umasikini duniani' GCAP pamoja na kampeini ya Milenia ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa hatua ya Oktoba 17 hadi 19 ilitoa ujumbe kwa viongozi wa duania kuwa raia wamechoka na hawatakaa tuu ikiwa ahadi zilizotolewa za kuutokomeza umaskani hazimizwi.

Yeye Askofu Desmond Tutu mwenyekiti wa kundi la wazee ambalo ni mkusanyiko wa marais wa zamani,wale waliopewa tuzo la Nobel,wafanya biashara pamoja na wahisani ambao huchangia mambo yao ya hekima, wanaotoa ushauri pamoja na maelekezo ya kutanzua baadhi ya matatizo ya dunia,anasema kuwa kampeini hiyo ilikuwa tamko la azma ya dunia katika vita vya kukomesha unyanyasaji mbaya wa umaskini.

Aidha amesema kuwa watu millioni 116 wametaka haki ya kupewa chakula,kuhudumiwa kiafya, kupewa elimu inayofaa pamoja na ajira.

Amesema kuwa watu hao millioni 116 wameshikamana ili kuuondoa umaskani,na kuongeza kuwa ujumbe huo ni lazima usikilizwe na viongozi wote kwani hauwezi kupuuzwa.

Mwenyekiti mwenza wa shirika la GCAP Kumi Naidoo amesem akuwa ni muhimu kuwashirikisha watu aliowaita 'wa kawaida' ili waweze kujihisi kama washirika kaztika kutafuta mbinu za kuboresha maisha yao.Aliongeza kuwa katika karibu kila nchi duniani pengo kati ya maskani na tajiri linazidi kuongezeka kwa haraka na pia pengo kati nchi maskani na nchi tajiri nalo ninaongezeka.

Hisia za watu kuchoshwa na serikali zilidhihirishwa w wakati wa sherehe za kauli mbiu ya 'jitokeze na uchukue hatua' kote Afrika wakati wananchi hao walipowataka watunga sera kuchangia juhudi zenye nia ya kupunguza umaskani,vifo vya watoto,kuboresha elimu pamoja na vifo vya mama waja wazito wakati wakijifungua,kukuiza usawa wa jinsia, pamoja na kuwaendeleza akina mama,kuweka mazingira sawa na pia kukabiliana dhidi ya UKIMWI na magonjwa mengine sugu ifikapo mwaka wa 2015.

Mfano nchini Malawi watu laki sita waliitaka serikali kuwajibika zaidi.Nchini Rwanda, rais Paul Kagame,aliungana na watu 10,000 ambao walisimama dhidi ya umaskanini katika uwanja wa Rubavu katika mkoa wa magharibi mwa nchi hiyo. Aliwataka watumie amani na usalama walivyopigania,kuvitumia kama msingi wa kupigana dhidi ya umaskani na kuletea taifa maendeleo.

Wanaharakati sio tu waliziomba serikali kuwasaidia katika juhudi zao za kupambana dhidi ya umaskini, lakini pia na viongozi wa kidini.Nchini Misri mamilioni walisimama misikitini,huku nchini nigeria,Sultan wa Sokoto,aliungana na watu 20,000 katika jimbo maskini nchini humo la Jigawa,kutoa mwito wa kuwawezesha akina mama na makundi mengine yasio na uwezo kujiimarisha kupitia mipango ya kuwapa mbinu hizo na pia kuwawezesha kupata mikopo ili makundi hayo yaweze kujiendeleza.

 • Tarehe 31.10.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Fkf2
 • Tarehe 31.10.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Fkf2
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com