Pembe ya Afrika -vita vinatishia kuzagaa | Magazetini | DW | 27.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Pembe ya Afrika -vita vinatishia kuzagaa

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo walituwama zaidi juu ya mada 2:hukumu ya kifo kuthibtishwa dhidi ya Saddam Hussein nchini Irak na vita nchini Somalia kati ya Ethiopia na wafuasi wa M ahkama za kiislamu.

NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG laandika:

“Katika Pembe ya Afrika msiba unanukia.Ikiwa mnamo siku chache tu za vita kati ya Ethiopia na Somalia watu 1000 wanasemekana wameuwawa,bahari ya damu yaweza kuchukua kipimo cha kutisha kabisa.

Ushindi dhidi ya magaidi wanaoshukiwa ni wafuasi wa Al Qaeda,ni vigumu kupatikana kijeshi.Na ukweli huu wa mambo, hautabdilishwa na nguvu kubwa za kijeshi za Ethiopia.

Turufu ya kisiasa ndio yafaa hapa kutupwa mezani.La sihivyo, yafaa kuhofia katika pembe ya Afrika kunapandishwa mbegu mpya za ugaidi unaoshikamana na jazba za chuki za kidini.”Ni maoni ya NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG.

Ama gazeti la Kölner Stadt Anzeiger linaelezea wasi wasi sawa na huo linapoandika:

“Nusu mwaka baada ya wafuasi wa kiislamu wenye siasa kali kuuteka mji mkuu Mogadishu,ulimwengu umezinduka kwa kujiingiza kijeshi Ethiopia nchini Somalia, ni hatari gain inatokota huko.Ushindi wa hivi sasa wa majeshi ya Ethiopia na wa serikali ya Somalia hausemi mengi.

Kwani, huko kunatokota vita virefu vya wanamgambo ambavyo tayari vimeshachukua sura ya kidini.Vita kati ya El Kaida na Ethiopia vinatishia sasa kuripuka na huenda vikageuka vita kati ya wakristu na waislamu ambavyo athari zake zaweza kuligawa bara zima la Afrika.”laonya gazeti la KÖLNER-STADT –ANZEIGER linalochapishwa mjini Cologne.

Gazeti la FRAKNFURTER RUNDSCHAU linasema:

„Ethiopia sasa imenadi vita vya mabomu majirani zake wa kiislamu.Wafuasi hao wa kiislamu wa kisomali wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo ambayo kwa sehemu kubwa ni jangwa.Na hii imezitia wahka Marekani,Ethiopia na imewafurahisha baadhi ya majirani.

Kambi zote mbili, ladai gazeti-tangu ile ilioingiwa na wasi wasi hata ile inaowaungamkono waislamu,zimejiingiza kati kwa nguvu katika mgogoro huu tangu kwa kulishia silaha hata na fedha.

Katika kambi moja, waislamu nchini Somalia wanaungwamkono sio tu na Eritrea-hasimu mkubwa wa Ethiopia,ambayo imeshakwenda nayo vitani,bali pia Djibouti,Libya,Misri,Saudi Arabia,Syria na Iran.Kwa muujibu wa ripoti ya UM zinatoa silaha na fedha .

Muungano wa kambi hizo mbili ukikutana katika changamoto ,basi mtu afaa kujiandaa kuzuka mripuko mkubwa.“

DIE WELT linatoa mafungamano ya kutumika jeshi la Ujerumani-Bundeswehr nchi za nje:

Laandika:

Si wanasiasa wa kijerumani tu wanaochomoka haraka panapozuka machafuko kudai kupelekwa jeshi kuzima moto.Hali kama hii ilionekana katika migogoro ya Balkan,nchini Afghanistan na pia Mashariki ya kati.Shauku ya kutojiingiza kijeshi inapungua na kutokana na kutozuka matatizo kwa kujiingiza Kongo,itaendelea kutopungua.

Maeneo mengine ya Afrika yanaanza sasa kukodolewa macho:Somalia ambako jeshi la Ujerumani tayari 1993 na 1994 liliweza kukusanya maarifa.

Hayakuwa lakini maarifa mazuri,kwani wanajeshi 30.000 wa kimataifa hawakumudu kumtuliza shetani humo nchini.Hali hii yafaa kuwazindua wote ambao wangeota ndoto ya kupeleka wanajeshi katika jangwa la Somalia.“-laonya DIE WELT.

Likitubadilishia mada,gazeti la WESTFÄLISCHEN NACHRICHTEN lazungumzia hukumu ya mahkama ya rufaa aliokatiwa Saddam Hussein nchini Irak hapo jana:Gazeti laonya:

„Marekani yafaa kutoshangiria hukumu hiyo.Kufurahia huko ni kujidanganya,kwani kwa jicho la umma wa wairaki ambao wengi wao wameikaribisha ,imetolewa maanani kwamba haikupitishwa na Mahkama huru.Kwa upande mwengine, hukumu ya kumnyonga Saddam itachimba zaidi kaburi kati ya madhehebu hasimu za washiia na wasunni.Na hilo ndilo jambo la mwisho ambalo serikali inayoregarega ya Irak na wanajeshi wa Marekani huko wangelihitaji.“