1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pele na Ronaldo wapongezana kwa rekodi ya ufungaji mabao

Bruce Amani
15 Machi 2021

Cristiano Ronaldo alimsifu Pele bada ya kuipiku rekodi ya nguli huyo wa Brazil ya upachikaji mabao katika mechi rasmi, kwa kufunga hat trick katika ushindi wa Juventus wa 3 – 1 dhidi ya Cagliari mechi ya Serie A

https://p.dw.com/p/3qetv
Cristiano Ronaldo 2009 - FIFA Fussballer des Jahres
Picha: Getty Images/AFP/J. Klamar

Cristiano Ronaldo alimsifu Pele bada ya kuipiku rekodi ya nguli huyo wa Brazil ya upachikaji mabao katika mechi rasmi, kwa kufunga hat trick katika ushindi wa Juventus wa 3 – 1 dhidi ya Cagliari jana kwenye mechi ya ligi kuu ya Italia. Pele ana rekodi ya mabao 767.

CR7 aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa ana pongezi za kudumu kwa Pele na heshima ya kandanda la katikati ya karne ya 20….na baada ya kufikisha bao lake la 770 katika Maisha yake ya kandanda, maneno yangu ya kwanza yanakwenda moja kwa moja kwa Pele. Hakuna mchezaji yeyote duniani ambaye hajakuzwa akisikiliza hadithi kuhusu mechi za Pele, mabao yake, an mafanikio yake na mimi ni miongoni mwao.

Pele aliisaidia Brazil kushinda Kombe la Dunia la 1958, 1962 na 1970. Pele naye alichukua fursa na kumpingeza Ronaldo. Aliandika "maisha ni safari moja. Kila mmoja anatengeneza safari yake. Na unaendelea kuwa na safari nzuri sana. Ninavutiwa nawe sana, napenda kukutizama ukicheza na hii sio siri kwa yeyote.” "Hongera kwa kuvunja rekodi yangu ya mabao katika mechi rasmi. Nasikitika tu kwamba sitaweza kukuwa nawe ili kukukumbatia leo.”

AFP, DPA, AP, Reuters