1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paul Mackenzie afikishwa mahakamani kwa tuhuma za ugaidi

8 Julai 2024

Mhubiri wa kidini nchini Kenya anayetuhumiwa kuwaamuru wafuasi wake wafunge kula na kunywa hadi kufa amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za ugaidi kutokana na vifo vya wafuasi wake zaidi ya 400

https://p.dw.com/p/4i1bV
Afrika Mombasa Paul Mackenzie
kiongozi wa dhehebu tata la kidini Paul Mackenzie Picha: Halima Gongo/DW

Paul Nthenge Mackenzie aliyejinadi kuwa mchungaji  amefikishwa mahakamani katika mji wa bandari wa Mombasa pamoja na washtakiwa wengine 94. 

Watu hao wanakabiliwa pia na mashtaka ya mauaji, kuua bila kukusudia, utekaji nyara, mateso na ukatili dhidi ya watoto. Mwezi Januari, Mackenzie na wenzake walikana mashtaka hayo ya ugaidi.

Miili ya wahanga wa Shakahola yatolewa kwa familia Kenya

Mackenzie, ambaye alikamatwa mwezi Aprili mwaka jana, anadaiwa kuwachochea wafuasi wake kujizuia kula hadi kufa ili waweze kukutana na Yesu Kristo.