1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Patashika kati ya Colombia-Ecuador na Venezuela

6 Machi 2008

Mvutano mpakani kati ya nchi 3 za Amerika kusini unazidi kupambamoto huku Ecuador na Venezuela zikituma majeshi yao mpakani na colombia.

https://p.dw.com/p/DJLQ
Rafael Correa und Hugo ChavezPicha: AP

Mvutano kati ya Colombia kwa upande mmoja na jirani zake Ecuador na Venezuela kwa upande wapili huko Amerika kusini,unazidi kupambamoto.

Ecuador na Venezuela zimetuma majeshi yao mpakani na Colombia. Colombia nayo imeungwamkono na mshirika wake Marekani.

Chanzo cha balaa hili ni majeshi ya Colombia kuvuka mpaka na kuingia Ecuador hivi majuzi na kuwahujumu waasi wa FARC huku rais wa Colombia akidai amepata ushahidi wa komputa unaoonesha majirani zake hao 2-Ecuador na Venezuela zinawafadhili waasi wa FARC kwa fedha.

Hujuma ya majeshi ya Colombia hapo jumamosi katika kambi ya waasi wa mrengo wa shoto -FARC ndani kidogo ya ardhi ya Ecuador na kumuua makamo- kiongozi wa jeshi hilo la waasi ,

Kumeongoza katika msukosuko wa kibalozi kati ya Colombia na majirani zake wawili waliovunja uhusiano huo .

Colombia inadai kwamba baada ya shambulio lake imekamata komputa za waasi hao imepata ushahidi kwamba nchi jirani za Ecuador na Venezuela zimekuwa zikiwafadhili waasi kwa misaada wa dala milioni 300-waasi wanaopigana vita kitambo kirefu na serikali ya Bogota.

Tangu Quito na Caracas zinakanusha vikali tuhuma hizo na zikawatimua nchini mwao mabalozi wa Colombia na kuvunja usuhuba wa kibalozi.

Ecuador na Venezuela zimepeleka sasa majeshi yao mpakani na Colombia ambayo nayo imeungwamkono na marekani katika ubishi wake na Ecuador na Venezuela.

Maafisa wa kijeshi wa Venezuela inayoongozwa na mwanama vikosi 10 vikiwa na wanajeshi hadi 6,000 vimepelekwa mpakani na Colombia na hadi 90 % wameshawasili huko.

Makamo-rais wa Colombia –Francisco Santos akijibisha hatua ya jirani zake hao 2 ,amesema mjini Brussels,Ubelgiji na ninamnukulu,

“Hatutumi majeshi zaidi ya yale yaliopo tayari huko mpakani.”.

Licha ya kupambamoto kwa hali ya mambo,Ikulu ya Marekani imesema ni mapema kidogo ni mapema sasa kuzingatia msaada wa kijeshi kwa mshirika wake Colombia.Rais wa Colombia Alvaro Uribe,ametoa mwito kutaka rais Chavez wa Venezuela afikishwe kwenye Mahkama ya Kimataifa inayowashughulikia wahalifu akimtuhumu amewafadhili waasi wa jeshi la kimapinduzi la waasi wa Colombia (FARC) kitita cha dala miliioni 300.

Marekani imeiomba Colombia kuiruhusu kuichunguza komputa hiyo inayoonesha ushahidi huo.Colombia,Marekani na Umoja wa Ulaya zinaliangalia jeshi hilo la waasi wa Colombia FARC ni chama cha magaidi.

Rais wa Ecuador Rafael Correa jana aliitaka Jumuiya ya kimataifa kulaani wazi wazi-dhahiri-shahiri kittendo cha Colombia cha kuvuka mpaka wake na kuhujumu.Jumuiya ya nchi 34 za Amerika imetoa taarifa kwa sauti moja ikisema Colombia imekiuka mamlaka ya Ecuador,lakini haikwenda umbali kama itakavyo Ecuador na Venezuela kkilaani wazi wazi kitendo hicho.