PARIS.Rais Denis Sassou Ngweso aonya juu ya mzozo wa Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 15.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS.Rais Denis Sassou Ngweso aonya juu ya mzozo wa Sudan

Mwenyekiti wa umoja wa nchi za Afrika rais Denis Sassou Ngweso wa Kongo Brazaville ameonya kuwa mzozo wa Sudan huenda ukatapakaza machafuko katika eneo zima la Afrika.

Wakati huo huo rais Ngweso ameutaka umoja wa mataifa upeleke jeshi la kulinda amani katika mipaka ya Chad na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Rais Ngweso aliyasema hayo mjini Paris baada ya kumaliza mkutano wake na rais Jaque Chirac wa Ufaransa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com