1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Wafanyakazi wa serikali wagoma

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CPav

Shinikizo dhidi ya mpango wa mageuzi wa rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa limezidi leo wakati maelfu ya wafanyakazi wa serikali walipojiunga na mgomo wa wafanyakazi wa reli ambao umekuwa ukiendelea kwa juma moja.

Walimu, wafanyakazi wa posta, wauguzi, maafisa wa kuongoza safari za ndege na wafanyakazi wengine wa serikali wamefanya mgomo wa siku moja kudai nyongeza za mishahara na kumalizika kwa mpango wa serikali kupunguza bajeti ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali.

Mgomo huo umesababisha shule nyingi kufungwa, hospitali kutoa huduma kidogo kwa wagonjwa na mawakala wa habari kukosa magazeti.