PARIS: Rais Abbas atoa wito kufufua utaratibu wa amani | Habari za Ulimwengu | DW | 24.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Rais Abbas atoa wito kufufua utaratibu wa amani

Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina,akikamilisha ziara yake barani Ulaya,amekutana na Rais wa Ufaransa,Jacques Chirac.Abbas ameomba msaada wa Chirac kufufua utaratibu wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina.Wakati huo huo,Chirac amesisitiza kuwa sasa ni wajibu wa Wapalestina kutekeleza kwa vitendo makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa,kati ya Fatah na Hamas,kama ilivyokubaliwa katika mkutano wa Mekka nchini Saudia Arabia.Amesema lililo muhimu kwa jumuiya ya kimataifa ni kutambua haki ya kuwepo taifa la Israel na pia makubaliano yaliokuwepo kati ya Waisraeli na Wapalestina yaheshimiwe.Hapo awali Rais Abbas alikuwa na majadiliano mjini London,Brussels na Berlin.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com