PARIS :Mwanawe Rais wa Chad afariki Paris | Habari za Ulimwengu | DW | 02.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS :Mwanawe Rais wa Chad afariki Paris

Mwanawe wa kiume wa Rais Idriss Deby wa Chad amepatikana akiwa amekufa katika eneo la kuegesha magari katika jingo alimokuwa akiishi.Kwa mujibu wa maafisa wa sheria kijana huyo alipatikana akiwa amekatwa kichwani na tukio hilo linafanyiwa uchunguzi wa mauaji.Mwili wake ulipatikana na msimamizi wa jengo hilo chini ya ngazi katika mtaa wa Coubevoie magharibi mwa mji wa Paris.

Maiti yake inatarajiwa kufanyiwa uchunguzi leo baadaye.Kulingana na duru za kisheria kijana huyo alifariki kwa njia ya ukatili na huenda aliuawa.Rais wa Chad alipewa habari hizo wakati akiwa anahudhuria mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Accra nchini Ghana.Hata hivyo kiongozi huyo hatakatiza ziara yake hiyo kwa mujibu wa msemaji wake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com