1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Mkutano kuhusu amani ya Mashariki ya Kati kufanyika leo

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBm3

Waziri wa mashauri ya kigeniwa Israel, Tzipi Livni, atakutana na mwenzake wa Morocco, Mohammed Benaissa, mjini Paris Ufaransa hii leo.

Afisa wa Morocco amesema viongozi hao watazungumzia njia za kuendeleza mchakato wa kutafuta amani ya Mashariki ya Kati.

Mazungumzo yao yatalenga kuuongezea nguvu mpango wa amani uliopendekwa na nchi za kiarabu na kuhakikisha majukumu ya kisiasa na kiuchumi ya Israel kwa mamlaka ya Palestina, yanatekelezwa.

Mpango wa amani uliosainiwa mjini Riyadh Saudi Arabia mnamo mwaka wa 2002 na kufufuliwa mwezi Machi mwaka huu, unapendekeza kujeresha mahusinao ya kawaida na Israel ikiwa taifa hilo la kiyahudi litaondoka kutoka kwa ardhi ya warabu iliyoiteka wakati wa vita vya mwaka wa 1967.

Mpango huo pia unakata kuundwe taifa huru la Palestina na wakimbizi wote wa kipalestina walio nchini Israel waruhusiwe kurejea makwao.

Mkutano wa mjini Paris utajadili njia za kuwahimiza Waisraeli na Wapalestina warejee kwenye meza ya mazungumzo. Waziri wa kigeni wa Israel, Tzipi Livni, atakutana pia na rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.