1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Kouchner aomba radhi

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVU

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa, Bernard Kouchner, ameomba radhi hadharani hii leo kwa kuyaingilia maswala ya ndani ya Irak.

Wakati wa ziara yake mjini Baghdad kati ya tarehe 19 na 21 mwezi huu, Kouchner alipendekeza waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki ajiuzulu.

Al Maliki jana aliitaka serikali ya Ufaransa iombe rasmi msamaha baada ya waziri Kouchner kuashiria katika toleo la jarida la Newsweek la Marekani kwamba waziri mkuu huyo wa kishia analazimika kuondoka madarakani.

Sambamba na hayo, waziri mkuu wa zamani wa Irak, Ayad Allawi, ametoa mwito kuundwe serikali mpya nchini Irak. Allawi amesema serikali ya sasa inayoongozwa na waziri mkuu, Nuri al Maliki, imeshindwa kumaliza machafuko.

´Kwa kweli sina shaka ikiwa ni mtu mzuri au la. Lakini natilia shaka mfumo wa makundi ya waasi au ukabila kwa kujaribu kupuuza mambo muhimu ambayo rais George W Bush na bunge la Congress linataka yatekelezwe na serikali ya Irak na sioni serikali hii ikiyatekeleza mambo hayo.´

Ayyad Allawi amesema anataka anataka kuikoa Irak na kazi inayofanywa na Marekani nchini humo.