PARIS : Idadi ya kubwa ya watu wajitokeza kupiga kura | Habari za Ulimwengu | DW | 22.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS : Idadi ya kubwa ya watu wajitokeza kupiga kura

Idadi kubwa ya watu imejitokeza katika masaa ya mwanzo ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa leo hii.

Kufikia mchana asilimia 31 ya wattu waliojiandikisha kupiga kura walikuwa tayari wamepiga kura zao.Idadi hiyo ni asilimia 10 zaidi iikilinganishwa na uchaguzi wa rais wa miaka mitano iliopita.

Ni wagombea wanne tu kati ya 12 wana nafasi ya kusonga mbele katika marudio ya uchaguzi yanayotegemewa kati ya wagombea wawili wakuu hapo tarehe 6 mwezi wa Mei.

Uchunguzi wa mwisho wa kura ya maoni umeonyesha mgombea wa sera za mrengo wa kulia Nicolas Sarkozy akiwa mbele kwa asilimia chache dhidi ya mgombea wa kisoshalisti Bibi. Segolene Royal akifuatiwa kwa karibu na mgombea wa sera za wastani Francois Bayrou na kiongozi wa sera kali za mrengo wa kulia Jean- Marie le Pen.

Uchaguzi huo wa kurithi nafasi ya Rais Jaques Chirac umekuwa ukidhibitiwa na masuala ya madeni ya serikali,ukosefu wa ajira na kutoridhika kijamii katika vtongoji vya wahamiaji.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com