PARIS: Basi mbili zachomwa moto na wafanya ghasia | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Basi mbili zachomwa moto na wafanya ghasia

Watu waliokuwa na silaha wamechoma moto mabasi mawili katika kitongoji kimoja katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, mwaka moja baada ya kutokea machafuko kufuatia vifo vya vijana wawili waliokumbwa na umeme katika maficho yao wakiikimbia polisi. Polisi wamesema watu wawili waliokuwa na silaha, waliingia jana jioni katika basi moja karibu na kituo cha treni cha Seine Saint-Denis mjini Paris na kuwalazimisha abiria wote pamoja na dereva kutoka ndani ya basi kabla ya kulitia moto.

Kwa uchache basi 5 zimeshashambuliwa katika vitongoji vinavyokaliwa na watu maskini mjini Paris tangu jumapili iliopita. Tangu ijumaa, serikali ya Ufaransa imeongeza polisi 4,000 kuimarisha usalama. Mwaka uliopita, gari zaidi ya 10,000 na gorofa kiasi ya 300 zilichomwa moto na waandamanaji katika machafuko yaliodumu wiki tatu mfululizo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com