PARIS: Amri mpya yazuia kuvuta sehemu fulani hadharani | Habari za Ulimwengu | DW | 01.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Amri mpya yazuia kuvuta sehemu fulani hadharani

Amri ya kuzuia kuvuta sehemu fulani za hadhara imeanza kutumika leo hii nchini Ufaransa.Sasa ni marufuku kuvuta katika hospitali,shuleni,ofisini vilabu vya spoti na katika vyombo vyote vya usafiri wa umma.Yeyote atakaekwenda kinyume na amri hiyo ataweza kupigwa faini ya hadi Euro 135.Sehemu ya pili ya amri hiyo itaanza kutumika mwanzo wa mwaka 2008 katika maeneo ambayo hivi sasa hayahusiki na sheria mpya.Miongoni mwa maeneo hayo ni mikahawa,mahala pa chakula,kwenye disko na hata majengo ya kucheza kamari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com