1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo XIV kuongoza Misa ya kwanza ya Krismasi

24 Desemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV atasherehekea Misa yake ya kwanza ya Krismasi katika Basilika ya Mtakatifu Petro usiku wa Krismasi.

https://p.dw.com/p/55vSU
Vatikan | Papat Leo XIV.
Baba Mtakatifu Leo amesema anarejea ombi lake kwa watu wote wenye nia njema kuifanya Krismasi kuwa siku ya amani.Picha: Vatican Media/ZUMA Press/IMAGO

Inatarajiwa kwamba kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki atazungumza dhidi ya vita na vurugu, na kukumbuka mateso ya binadamu.

Papa Leo tayari ametoa matamko kadhaa akitoa wito wa amani na upatanisho, na kuwakumbuka waathiriwa wa vita duniani kote.

Baba Mtakatifu Leo amesema anarejea ombi lake kwa watu wote wenye nia njema kuifanya Krismasi kuwa siku ya amani, kwa angalau kuonesha heshima kwa siku hiyo ya kuzaliwa Yesu Kristo.

Wakristo duniani watasherehekea sikukuu ya Krismasi hapo kesho kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu zaidi miaka 2000 iliyopita.