1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedict akosolewa kutokana na uamuzi wake wa kumrejesha kundini askofu aliyetengwa.

Sekione Kitojo4 Februari 2009

Uamuzi wa kumrejesha kundini askofu aliyetengwa kutokana na kukana kutokea mauaji ya halaiki ya Wayahudi Holocaust umesababisha ukosoaji mkubwa dhidi yake.

https://p.dw.com/p/GnEf
Pope Benedict akiwa katika kanisa la mtakatifu Joseph, katika Vatican.Picha: picture-alliance/ dpa



Uamuzi wa Kiongozi mkuu wa Kaniasa katoliki duniani Papa Benedict 16, wa kumrejesha kundini katika kanisa hilo askofu ambaye amekuwa akikana mauaji makubwa ya kikatili dhidi ya Wayahudi yanayojulikana kama Holocaust , umeleta hali ya kuchukiza nchini Ujerumani nchi ambayo anatoka Papa. Hatimaye hata kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mwenyekiti wa chama cha SPD Franz Müntefering wamemkosoa Papa.



Wakati Joseph Karnidali Ratzinger anatimiza karibu miaka minne tangu kuchaguliwa , kumekuwa na mengi, hususan wachunguzi waandamizi wameshangazwa. Hakuna ubishi kwamba hadi sasa Ratzinger ni mmoja kati ya wanazuoni wenye upeo wa juu kabisa katika elimu ya kidini katika kanisa Katoliki katika wakati wetu.

Lakini pamoja na mambo mengine, kumuingiza Mjerumani ambaye duniani kote anaonekana kuwa ni mhalifu wa wakati wa utawala wa Kinazi katika mauaji ya Wayahudi ya Holocaust katika uongozi wa taasisi inayoheshimika hili haliwezekani. Na zaidi ya hayo Ratzinger binafsi ni mmoja wa jamii ya vijana , wakati akiwa mdogo bado, aliingizwa katika jeshi la Hitler kwenda kupigana vita, na kuwa katika upande wa watu wabaya.

Uteuzi wa Ratzinger kuwa Papa ulionekana wakati ule kuwa ni kuwarejesha Wajerumani katika ulimwengu wa kistaarabu.

Kutokana na kosa hili kubwa hivi sasa , hadhi ya Papa Benedict, Papa kutoka Ujerumani , imeingia katika shaka kubwa, kwamba chuki dhidi ya Wayahudi katika kanisa Katoliki inakubalika na ukanaji wa mauaji ya Wayahudi ya Holocaust utakuwa unavumiliwa.

Hata hivyo yeyote aliyesoma maandishi ya Joseph Ratzinger pamoja na matamshi yote ya Papa katika muda wa siku kumi zilizopita ameweza kufahamu kuwa , yote hayo si kweli.

Kitu gani kimetokea, Benedict 16, ameondoa hali ya kutengwa dhidi ya maaskofu wanne, watu ambao kwa muda wa miaka 20 tangu mtangulizi wa Papa huyu wa sasa kuwatengwa kutoka katika kanisa Katoliki. Sababu ya kufanya hivyo ni kuwaweka wakfu maaskofu hao bila ya kupata kibali cha makao makuu ya kanisa, kitu ambacho ni wazi kuwa ni kinyume na sheria za kanisa na kutokana na hayo ni kinyume na kanisa Katoliki.

Kutokana na kufutwa kwa hatua ya kutengwa , watu hao wanne sasa wanaweza kushiriki katika ushirika mtakatifu, yaani sacramenti, pia wanaweza kushiriki katika misa ama kuungama.

Kwa hali yoyote ile watu hao wanne wamerejeshwa katika hali ya kawaida. Wamerejeshwa tena katika utawala kama maaskofu wa kanisa Katoliki na mawazo yao yatatumika katika hatua baina ya ukatoliki na dini ya Kiyahudi, na kwamba hii itakuwa ni mtazamo wa jumla wa kanisa Katoliki.

Tatizo lakini liko sehemu nyingine , uamuzi wa Papa kwa mtazamo wa viongozi wengine wa kanisa na uwajibikaji juu ya umoja wa kanisa huenda unaeleweka kuwa unaweza kuwa una taabu kueleweka, sio ndani ya kanisa, lakini kama ukosoaji unavyoonekana kuwa mkubwa dhidi ya Papa kutoka kwa maaskofu na kupindukia hapo.