1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PANAMA-CITY: Mfereji wa Panama kupanuliwa

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSs

Nchini Panama kumefanywa sherehe za kuzindua kazi za kupanua mfereji wa Panama katika mradi ulio mkubwa kabisa nchini humo.Mfereji wa Panama uliojengwa na Marekani na kuunganisha bahari za Atlantik na Pacifik,unatazamiwa kupanuliwa,ili meli kubwa za kusafirisha makontena na mafuta na hata meli za utalii ziweze kupitia njia hiyo.Kazi za ujenzi huo zinatazamiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka 2015.Wananchi wa Panama,katika kura ya maoni iliyopigwa mwezi Oktoba mwaka jana, waliidhinisha gharama za mradi huo, ikitathiminiwa kuwa ni zaidi ya Euro bilioni 3,8.