Pakistan-Sharif kukamatwa akiwasili | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 24.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Pakistan-Sharif kukamatwa akiwasili

Mambo yamegeuka kwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif .Mahkama jana iliamua aweza kurudi nyumbani kutoka uhamishoni.

Waziri-mkuu wa zamani wa Pakistan,Nawaz Sharif anaeishi uhamishoni mjini London na ambae Mahkama Kuu ya Pakistan ilisema jana aweza kurejea nchini,huenda akakamatwa mara tu akiwasili Pakistan-mwanasheria mkuu wa serikali-Malik Abdul Qayyum amearifu leo.

Mbali na uwezekano wa kutiwa nguvuni,wakili huyo amesema pia hataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi ujao kwavile, hukumu aliyopitishiwa juu ya njama ya utekajinyara ndege bado ina nguvu.Hafai kugombea uchaguzi ujao chini ya kifungu cha sheria nambari 62 cha katiba ya Pakistan,alisema Qayyum.

Abdul Qayyum amesema adhabu ya faini ya Rupia milioni 500 haikubatilishwa na fedha hizo zitapatikana kwa kunyakuliwa nyumba yake na serikali.

Nawaz Sharif alikutikana na hatia katika kesi ya utekajinyara-ndege na akahukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha,lakini adhabu hiyo ilifutwa kwa sharti kuwa alikubali kuondoka nchini kuishi uhamishoni kwa kipindi cha miaka 10.Sasa ikiwa ameamua kurejea nchini,serikali ya Pakistan chini ya hasimu wake jamadari Musharraf,yaweza pia kubadili msimamo wake.

Waziri mkuu wa sasa wa Pakistan,Shaukat Azizi kisheria,adai Qayyum, aweza kumshauri rais Musharraf kurejesha adhabu ya kiffungo korokoroni.

Kulikuwapo jana shangwe na shamra shamra baada ya Mahkama Kuu ya Pakistan,kupitisha kuwa masharti ya kumhamishia nchi za nje waziri mkuu Nawaz Sharif aliopewa na jamadari Musharraf baada ya kumpindua madarakani hapo 1999 ni batili.

Uwezekano wa kurejea nchini Pakistan kwa Nawaz Sharif kunaangaliwa na wachunguzi wa kisiasa ni pigo kali kwa utawala wa kijeshi wa jamadari Musharraf anaetapia kubakia madarakani kwa kipindi kingine cha miaka 5 kabla ya uchaguzi mkuu wa oktoba 15.

Sharif mwenye umri wa miaka 57 ametumika mara 2 kama waziri mkuu wa Pakistan na amebakia mwanasiasa maarufu wa chama cha Pakistan Muslim League.Mpinzani mwenzake ni waziri-mkuu mwengine wa zamani Benazir Bhutto,anaesemekana akifanya mazungumzo faraghani na jamadari Musharraf ili kugawana madaraka.

Nawaz Sharif lakini amepinga ushirikiano wowote na jamadari Musharraf na ametoa mashati yake anayotaka yatimizwe nchini Pakistan:

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com