​​​​​​​Pacquiao kutupiana makonde na Khan | Michezo | DW | 27.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

​​​​​​​Pacquiao kutupiana makonde na Khan

Katika masumbwi bondia mfilipino Manny Pacquiao na bondia muingereza Amir Khan wamekubalianan kurushiana makonde mnamo April 23, mwaka huu

Hii ni baada ya kuwepo kwa taarifa tata kuhusiana na mpambano kati ya mabondia hao. Manny Pacquiao aliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa mazungumzo kati ya kundi lake la timu Pacquiao na timu Khan yamezaa matunda ambapo pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kufanyika mpambano huo. Sehemu ambako mpamabano huo wa masumbwi utafanyika bado haijatajwa ingawa taarifa za awali kutoka upande wa Pacquiao zinaonyesha kuwa pambano hilo litapigwa katika Jamhuri ya Falme za Kiarabu  United Arab Emirates.

Manny Pacquiao mwenye umri wa miaka 38 hivi sasa mwaka jana alitangaza kutundika gloves darini na kuachana na masumbwi kabla ya  kubadilisha uamuzi huo baada ya kumdunda Jessie Vargas mjini Las Vegas Novemba mwaka jana na kusema bado anajiona ni kijana na anaweza bado kuendelea kupanda ulingoni.

Mwandishi: Isaac Gamba
Mhariri: Yusuf Saumu