1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Outtara asema yuko tayari kuendelea kuhudumu kama rais

9 Januari 2025

Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara amesema kwamba angependa kuendelea kuhudumu kama rais wa nchi hiyo, ingawa amesisitiza kuwa chama chake bado hakijafanya uamuzi kuhusu mgombea atakayesimama katika uchaguzi ujao.

https://p.dw.com/p/4ozgP
Alassane Outtara amesema leo kwamba angependa kuendelea kuhudumu kama rais wa nchi hiyo
Alassane Outtara amesema leo kwamba angependa kuendelea kuhudumu kama rais wa nchi hiyoPicha: Denis Balibouse/KEYSTONE/REUTERS/POOL/dpa/picture alliance

Katika hotuba yake kwa wanadiplomasia mjini Abidjan, Outtara mwenye umri wa miaka 83, ameeleza kuwa ana afya njema na mwenye hamu ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa nchi yake.

Kiongozi huyo, aliyechaguliwa tena kwa muhula wa tatu katika uchaguzi uliozua utata mnamo mwaka 2020, hapo awali alionyesha utayari wa kustaafu, lakini akapendekeza kwamba washindani wake wazee pia wanapaswa kujiondoa kwenye siasa.