1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ouattara, Gbagbo wakubaliana kumaliza tofauti

Sudi Mnette
28 Julai 2021

Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo amekutana na rais wa sasa wa taifa hilo Alassane Ouattara, ikiwa ni zaidi ya muongo mmoja baada ya vurugu za uchaguzi zilizolizonga taifa hilo la Afrika Magharibi.

https://p.dw.com/p/3y9YC
Elfenbeinküste I Alassane Ouattara und  Laurent Gbagbo in Abidjan
Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

 

Mkutano huo uliotarajiwa kwa kiwango kikubwa unatajwa kuwa ni jaribio la kupunguza mvutano wa kisiasa, ambazo zimekuwepo nchini Ivory Coast tangu kufanyika mkutano wao wa mwisho kwa viongozi hao zaidi ya muongo mmoja uliopita, pale ambapo Ouattara alipomshinda Gbagbo katika uchaguzi wa rais.

Akizungumza baada ya mkutano wao, Ouattara alisema wameona ni muhimu kurejesha hali ya uaminifu baina yao, ili raia wa taifa hilo wakaingia katika mapatano na hasa katika kuaminiana kwa kila mmoja. zaidi rais huyo alisema "Tumeamua ni muhimu kujenga hali ya kujiamini, na kutafuta njia ya maridhiano ya Waivorycoast, hili ndio jambo la msingi, na kuamiana kwa kila mmoja wetu. Matukio yaliopita yakuwa na machungu. Kulikuwa na vifo vingi. Lazima tuyasahau hayo na kutazama hatma, kwa mshikamano na mapatano."

Gbagbo ataka wafungwa wa kisiasa waachiwe huru.

Elfenbeinküste I Alassane Ouattara und  Laurent Gbagbo in Abidjan
Rais Alassane Ouattara na Laurent GbagboPicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Ameongeza pia kwamba wamRais Ouattara wa Ivory Coast kukutana na hasimu wake Gbagboekubaliana kukutana tena katika majuma yajayo kwa lengo la kuondosha tofauti zao na kuweka kando yale yote yaliopita baina yao. Gbagbo kwa upande wake alisema angependa rais huyo awaachie huru wale waliokuwa wakimuunga mkono ambao kwa sasa wapo magerezani nchini humo. Gbagbo aliongeza "Tumezungumzia kwa namna gani lazima Ivory Coast isonge mbele, mambo gani yatapaswa kufanyiwa kazi, yapi tuyazungumze, tuyajadili."

Tangu awasili nchini humo,Gbagbo amekwishakutana na Henry Konan Bedie, rais wa zamani, ambae pia hasimu wake mwingine wa kisiasa. Lakini pia alikwenda katika kijiji chake cha asili huko mashariki ya kati ya taifa ya Ivory Coast pamoja na kuzuru Congo.

Gbagbo amerejea nchini Ivory Coast hivi karibuni baada ya Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ICC, kuyatupilia mbali mashtaka yake uhalifu dhidi ya binaadamu, ya vurugu za baada ya uchaguzi, ambazo zilisababisha watu 3,000 kuuwawa.

Katika uchaguzi wa 2010, Gbagbo aliyaktaa matokeo dhidi ya Ouattara, jambo ambalo lilisababisha mapigano makali kati ya wafuwasi wao. Mwaka 2011 alipelekwa mjini The Hague. Lakini baadae 2019 akaachiwa huru kwa kutokukutwa na hatia. Na baadae aliruhusiwa kurejea nyumbani Ubelgiji, ambako alikuwa akiishi.

Vyanzo: DPA/AP