1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ouattara ahutubia taifa

Halima Nyanza8 Aprili 2011

Rais anayetambuliwa kimataifa nchini Cote d'Ivoire, Alassane Ouattara ameagiza kuwekwa vizuizi katika makaazi ya Rais anayeng'ang'ania madarakani Laurent Gbagbo ambako bado amejificha.

https://p.dw.com/p/10phu
Rais wa Cote d'Ivoire anayetambuliwa kimataifa Alassane OuattaraPicha: AP

Akizungumza jana usiku kupitia televisheni ya nchi hiyo, Ouattara ameyatolea wito pia majeshi yake kudumisha utaratibu katika mji mkuu wa nchi hiyo Abidjan, ambako wanamgambo wanaorandaranda katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi na kufanya mashambulio yasiyo na mpangilio maalumu.

Elfenbeinküste Unruhen nach Wahl
Mitaa ya mji wa Abidjan, unaokabiliwa na mapiganoPicha: AP

Katika hatua nyingine katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki Moon amemtaka Rais Gbagbo kuachia madaraka mapema kabla ya kuchelewa.

Amesema hiyo ni fursa ya mwisho kwa gbagbo kuondoka vizuri katika nafasi hiyo na kumkabidhi madaraka Ouattara.

Elfenbeinküste Gefangene 06.04.2011
Wanajeshi wa Ouattara wakiimarisha ulinzi kwa kuwakamata watu wanaohisiwa kuwa ni wapiganaji.Picha: AP

Wakati huohuo, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d'Ivoire umesema utamkamata gbagbo akiwa hai na kumfungulia mashtaka.

Ouattara amekuwa akisisitiza juu ya Gbagbo kukamatwa akiwa hai, licha ya kwamba majeshi yake yamekuwa yakitoa upinzani mkali.