1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oscar Pistorius kuanza mazoezi mepesi

28 Juni 2013

Oscar Pistorius ataanza kufanya mazoezi mepesi ili kumsaidia kujiandaa kwa kesi yake ya mauaji na kukabiliana na dhiki ya kumuuwa mchumbake Reeva Steenkamp. Mazoezi hayo siyo ya kushiriki mashindano yoyote

https://p.dw.com/p/18yDc
South Africa's Oscar Pistorius starts his men's 400m round 1 heats at the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium August 4, 2012. REUTERS/Dylan Martinez (BRITAIN - Tags: OLYMPICS SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Olympia London 2012 Leichtathletik Oscar PistoriusPicha: Reuters

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Pistorius imesema mwanariadha huyo anayetumia miguu ya kubandikwa ameamua kufanya mazoezi mepesi kwa saa chache kila wikiili kujiandaa kiakili.

Pistorius amesema hatashiriki katika mashindano yoyote mwaka huu wote wa 2013 wakati akikabiliwa na kesi inayooenekana kuchukua muda mrefu ya kumpiga risasi na kumuua Steenkamp, lakini sasa anataka kufanya mazoezi ya mara kwa mara wakati kesi yake ikiendelea.

Kesi yake itaendelea Agosti 19, wakati waendesha mashitaka watakapoamua kama ana mashitaka ya kujibu au la, na tarehe ya kuanza rasmi kesi yake huenda ikawekwa mwezi Septemba au Oktoba. Pistorius mwenye umri wa miaka 26 anakanusha mauwaji ya Steenkamp akisema alimpiga risasi kimakosa kwa sababu alidhani ni mwizi aliyeingia nyumbani kwake. Kama atapatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia, atakabiliwa na adhabu ya kifungo cha chini cha miaka 25 gerezani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters

Mhariri: Yusuf Saumu