Oscar Pistorius afungwa miaka 5 gerezani | Michezo | DW | 21.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Oscar Pistorius afungwa miaka 5 gerezani

Mahakama nchini Afrika Kusini imemuhukumu kifungo cha miaka mitano gerezani, mwanariadha nyota wa michezo ya Olimpik, Oscar Pistorius kwa kosa la kumuuwa rafiki wake wa kike Reeva Steenkamp mwaka 2013.

Oscar Pistorius kommt zum Gericht 21.10.2014

Mwanariadha Oscar Pistorius akiwa kizimbani

Jaji aliekuiwa akiongoza kesi ya mwanariadha mwenye ulemavu wa miguu, Oscar Pistorius, Thokozile Masipa leo hii amemuhukumu kifungo hicho cha miaka mitano gerezani mwanariadha huyo kutokana na kosa la kumuuwa kwa kumpiga risasi rafiki wake wa kike Reeva Steenkamp, katika siku ya wapendanao mwaka uliopita.

Mkasa huo wa mauwaji ulitokea pale ambapo Pistorus alipoufyatulia risasi mlango wa choo, akiwa nyumbani kwake, na kubainika kuwa tukio hilo lilikuwa la bahati mbaya kwa kuwa alidhani marehemu kuwa alikuwa mwarifu wa nyakati za usiku.

Waendesha mashitaka walitaka hukumu kali

Oscar Pistorius Urteil 21.10.2014 Richterin Masipa

Jaji Thokizile Masipa alietoa hukumu ya Oscar

Jaji Masipa ametoa uamuzi huo baada ya kupitia hoja za upande wa waendesha mashitaka ambao walikuwa wakishinikiza au kutaka adhabu kali zaidi ya kifungo kwa mwanariadha huyo. Amekutwa na hatia ya kuuwa kwa kufanya mauwaji kwa uzembe.

Mwanaridha huyo nyota alismama barabara akisikiliza hukumu yake wakati jaji alipokuwa akiitangaza, na baadae akaiondoka katika chumba cha mahakama na kushuka ngazi kulekelea katika chumba ambacho amewekwa kwa muda kabla ya kwenda kutumika hukumu yake. Na kifungo hicho cha miaka mitano kinaanza mara moja.

Watalaamau katika masuala ya kisheria wanasema Oscar atatumikia kifungo cha wastani wa juu cha miaka mitano na upo uwezekano baada ya kutumika kifungo cha nyumbani baada ya miezi minane. Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya mwendesha mashitaka nchini Afrika Kusini, Nathi Mcube, ofisi hiyo bado haijatoa uamuzi wowote kama itaikatia rufa hukumu hiyo au la.

Msemaji huyo alisema ofisi hiyo imeskiitisha kwa mtuhumiwa huyo kuhusishwa na mauwaji, kwa hivyo wanaitathimini hukumu na wana siku 14 ya kujiridhisha kisheria kwa jinsi mchakatao huo ulivyofanyika na kwamba baada ya hapo watakuwa na uwezo wa kujua hatua ipi ifuate.

Hata hivyo Mcube amesema ana imani kwamba Waafrika Kusini watakuwa na imani na uamuzi wa Jaji Masipa dhidi ya Oscra Pistorius. Mmoja kati ya walikuwemo katika timu ya utetetezi ya mwanariadha huyo Roxanne Adams" alisema hana cha kuzungumza kwa wakati huu na hasa katika suala la ukazaji rufaa au la.

Lakini Adams aliongeza kwa hukumu hiyo inanonekana kama Pistorius atatumika kifungo cha miezi 10 gerezani, katika kifungo chake cha miaka 5 kabla hajapelekwa katika hatua ya kifungo cha nyumbani. Kaka wa mwanaridha huyo Carl alionekna akiwasukuma wandishi habari kwa nguvu wakati akisindikiza Adams nje ya mahakama.

Upande wa familia wamepokea vyema uamuzi wa kifungo cha mwanariadha huyo. Mwanasheria wa familia hiyo, Dup de Bruyn amesema wazazi wa Steenkamp wameridhishwa na uamuzi wa kifungo cha miaka mitano.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP/APE/DPA

Mhariri: Josephat Charo

DW inapendekeza